Sikumoja Mwantumu alipokuwa amekwenda kuteka maji mtoni, njiani alikutana na Bw. Jumbe ambaye alikuwa anakwenda kuangalia vibuyu vyake vya mnazi kama vimeingia pombe ya mnazi ambayo aliviweka jana alasili. Akamsabahi Mwantumu ambaye alikuwa yupo kwa mwendo wa haraka kidogo kuelekea mtoni. Mwantumu akasimama na kuitikia salamu ya Bwana Jumbe kwa adabu zote. Bwana Jumbe baada ya kusalimiana na Mwantumu, akampa tahadhari kuwa kuna mamba ambaye anashuka kutokea upande wa juu. Hivyo awe makini pindi anapochota maji sije akamkamata.
Mwantumu alimshukuru Bwana Jumbe na haraka akaendelea na safari yake ya kuelekea mtoni. Aliyakuta maji ni matulivu na vyura walikuwa wakiimba nyimbo za kufurahia maji na hali tulivu ya sehemu ile. Mwantumu kwa tahadhari kubwa akaingza mtungi wake katika maji na ghafla kabla ya kufanikiwa kuchota maji, mamba akamkamata nguo nakuanza kumvutia kwenye maji ya kina kirefu.
Bwana Jumbe hakuwa mbali sana na eneo lile ambalo mamba amemkamata Mwantumu, alikuja huku anakimbia nakupiga kelele, alimkuta mamba amekamata sketi ya mwantumu akiwa ameng'ang'ana kumvutia Mwantumu katika maji marefu. Bwana Jumbe akarukia kwenye maji nakuanza kupambana na mamba yule. Mamba akamwachia Mwantumu na kumdaka Bwana Jumbe mkono.
Je nini kitaendelea? Endelea kufuatilia ujue kama Bwana Jumbe alipona ama la!
No comments:
Post a Comment