Mkwayu alipanda farasi wake mweusi mwenye siha njema nakupotea machoni mwamfalme kuelekea katika kisiwa cha Mikwingwina kilichopotakribani kilometa 75 toka pale walipo. Mkwayu kabla yakuondoka alimweleza mfalme angerudi na lulu ndani ya siku 2 zikizidi wajue amepatwa na mabaya. Pia alichoma shale kwenye mti nakuutemea mate yake nakusema ilihali watu wote wakiwa wanasikia maneno yale kwamba, mshale ule ukidondoka wenyewe chini toka katika mti, basi nayeye atakuwa amekumbwa na mabaya huko aendako.
Usiku wa manane ulivuma upepo mkali sana katika ile sehemu waliyokuwa wamepumzika mfalme na kundi lake mpaka mahema yalikaribia kung'ooka kutokana na upepo uliokuwa unavuma. Mara baada ya dakika takribani arobaini na tano, upepo ulikoma na hali ilibakia katika haliyake ya kawaida. Mlinzi aliyekuwa ameshika zamu usikuhuo alipo kuwa anakagua usalama, alikutana na mshale uliokuwa umewekwa na Mkwayu umedondoka chini, haraka aliwaeleza wenzake na mfalme pia alijulishwa juu ya hali ile na kugundua mojakwamoja kuwa Mkwayu amekutwa na jambo baya huko alikokuwa amekwenda.
Akawaambia walinzi wake kuwa haiwezekani Lulu isispatikane na dhaihiri inaonyesha kuwa huko Mkwayu alipokwenda kunaupinzani mkubwa hivyo waondoke wote waende kuitafuta lulu kwani ingekuwa aibu kubwa sana kwa mfalme kushindwa kupeleka zawadi ya mtoto wake kipenzi Mboni.
Ilipotimia majira ya saa kumi na nusu tayari mfalme pamoja na watu wake walikuwa njiani kuelekea katika visiwa vya mikwingwina ili kumtafutia binti yake mpendwa zawadi aliyo ihiyo ihitaji ya lulu.
Ilipotimu majira ya saa saba hivi mchana mfalme paoja na watu wake walikuwa wamesha wasili ng'ambo yapili ya kivuko kuelekea katika kisiwa cha mikwingwina. Mfalme Mbezi alitoa kifaa maalumu cha kukatisha maji kilichounganishwa na nanga nzito ndogo nakufungwa ng'ambo ya kwanza kisha kufungwa katika kamba ndefu ngumu ya manila nene. Mathayo aliyekuwa mlinzi wa Mbezi alipewa jukumu la kwenda mpaka ng'ambo ya Mikwingwina na kisha kutafuta mtimkubwa afunge kwaajili ya kuvukia juu kwaajili ya mikono na kamba ya chini kwaajili ya kukanyaga kwa miguu yaani, kwakifupi kitendo cha kufunga kamba ng'ambo ya kwanza na ng'abo ya pili inaitwa NEMA. Baada ya zoezi lile kukamilika Mathayo alirudi ng'ambo ya kwanza ya mikwingwina na kumwambia Mfalme Mbezi kuwa zoezi limekamilika na hali ya kiusalama ipo madhubuti. Mfalme akaamrisha makamanda wawiliwawili wavuke kwenda kisiwani mikwingina kuleta lulu, Sufiani pamoja na Saidi walikabidhiwa vifaa vya kutendea kazi kama kisu cha almasi kwaajili ya kukatia madini ya lulu pamoja na upanga, mkuki pamoja na mishale kwaajili ya kujihami. Saidi na Sufiani walianza safari kwa pamoja mpaka ng'ambo ya pili salama. Walipokuwa njiani kuelekea kaskazini mwa Mikwingwina waliona nyoka aina ya chatu wapatao kama 500 hivi wakawazingira na kuwameza kwa fujo.

No comments:
Post a Comment