Monday, July 20, 2015

SITASAHAU MAISHANI.

Nilikuwa darasa latano kipindi hicho, nilikuwa mimi na wadogo zangu wawili. Kawaida yetu ilikuwa kila tukimaliza kula chakula cha usiku tunapumzika kidogo, halafu tunasali, na kama kuna mwenye homework anafanya na anaingia kitandani na kulala. Sikuhiyo baba alikuwa hajarudi kipindi nafanya homework baada ya kuwa tumemaliza kusali na mama pamoja na wadogo zangu walikuwa tayari wamesha lala. Takribani saa sita usiku baba akarudi akiwa chakali amelewa, alibisha hodi mama akaamka na kumfungulia, alikuwa mkali sijawahi kumwona baba yangu akiwa mkali vile, akamnasa mama makofi mbele yangu, mama aligumia kwa maumivu, hali ile iliniuma sana mpaka nikalia. Hakuishia hapo bali alimrushia mateke kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzake. Mama aliumia sana, nami sikuweza kuvumilia haliile, kipindi hicho tulikuwa tumeagizwa fimbo za kupeleka shuleni aina ya mikamilwa, nilichukua fimbo mkamilwa mmoja nikamfuata baba aliyekuwa amemwangusha mama chini nakuendelea kumpa makonde yasiyonaidadi. Kwahasira na nguvu nilimtiririshia baba mvua za fimbo mgongoni mpaka nayeye akapiga mayowe. Akamwacha mama na kuanza kunikimbiza, kwakuwa mlango ulikuwa haujafungwa nilitoka mbio nayeye yupo nyuma yangu anakuja mbio anikamate, nikakimbilia sehemu moja iliyokuwa imezibwa njia kwa miiba ya michongoma. Kwakuwa sehemu ile nilikuwa naijua nikairuka miba ile nayeye hakuwa akijua kama kuna miba, aliingia mzimamzima. Alikipata hakika. Nikahamia kwa rafiki yangu wiki nzima na mama akawaomba wazee watusuluhishe mimi na baba. Nilimwomba radhi baba na akanisamehe. Je nisingechukua maamuzi magumu kama hayo mamaangu siangeuwawa mbele yangu namwona?

1 comment: