Monday, July 20, 2015

SITASAHAU MAISHANI.

Nilikuwa darasa latano kipindi hicho, nilikuwa mimi na wadogo zangu wawili. Kawaida yetu ilikuwa kila tukimaliza kula chakula cha usiku tunapumzika kidogo, halafu tunasali, na kama kuna mwenye homework anafanya na anaingia kitandani na kulala. Sikuhiyo baba alikuwa hajarudi kipindi nafanya homework baada ya kuwa tumemaliza kusali na mama pamoja na wadogo zangu walikuwa tayari wamesha lala. Takribani saa sita usiku baba akarudi akiwa chakali amelewa, alibisha hodi mama akaamka na kumfungulia, alikuwa mkali sijawahi kumwona baba yangu akiwa mkali vile, akamnasa mama makofi mbele yangu, mama aligumia kwa maumivu, hali ile iliniuma sana mpaka nikalia. Hakuishia hapo bali alimrushia mateke kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzake. Mama aliumia sana, nami sikuweza kuvumilia haliile, kipindi hicho tulikuwa tumeagizwa fimbo za kupeleka shuleni aina ya mikamilwa, nilichukua fimbo mkamilwa mmoja nikamfuata baba aliyekuwa amemwangusha mama chini nakuendelea kumpa makonde yasiyonaidadi. Kwahasira na nguvu nilimtiririshia baba mvua za fimbo mgongoni mpaka nayeye akapiga mayowe. Akamwacha mama na kuanza kunikimbiza, kwakuwa mlango ulikuwa haujafungwa nilitoka mbio nayeye yupo nyuma yangu anakuja mbio anikamate, nikakimbilia sehemu moja iliyokuwa imezibwa njia kwa miiba ya michongoma. Kwakuwa sehemu ile nilikuwa naijua nikairuka miba ile nayeye hakuwa akijua kama kuna miba, aliingia mzimamzima. Alikipata hakika. Nikahamia kwa rafiki yangu wiki nzima na mama akawaomba wazee watusuluhishe mimi na baba. Nilimwomba radhi baba na akanisamehe. Je nisingechukua maamuzi magumu kama hayo mamaangu siangeuwawa mbele yangu namwona?

Sunday, July 19, 2015

MTOTO WA MFALME NA LULU - 3

Mfalme Mbezi alipoona kuwa walinzi wake hawarudi katika siku ileile aliyo wapangia, akaamua aongeze siku moja zaidi kuwasubiria na kama hawatafika aweze kufanya kitu ili kuhakikisha kuwa lulu ya binti yake inapatikana kwahali yoyote ile. Ilipofikia majira ya saakenda mfalme Mbezi alihisi kuwa huenda watuwake waliokuwa wamekwenda kisiwa cha mikwingwina wamep-atwa na mabaya. Akawaambia watuwake waliokuwa pamoja nae kuwa, ''Lulu kwaajili ya binti yangu nilazima ipatikane na sipo tayari kurudi Mgombezi bila lulu'' Akawaambia watu wake kuwa hakuna mtu atakayebakia ng'ambo yakisiwa cha Mikwingwina

WATOTO NI ZAWADI.

Sikumoja Mwantumu alipokuwa amekwenda kuteka maji mtoni, njiani alikutana na Bw. Jumbe ambaye alikuwa anakwenda kuangalia vibuyu vyake vya mnazi kama vimeingia pombe ya mnazi ambayo aliviweka jana alasili. Akamsabahi Mwantumu ambaye alikuwa yupo kwa mwendo wa haraka kidogo kuelekea mtoni. Mwantumu akasimama na kuitikia salamu ya Bwana Jumbe kwa adabu zote. Bwana Jumbe baada ya kusalimiana na Mwantumu, akampa tahadhari kuwa kuna mamba ambaye anashuka kutokea upande wa juu. Hivyo awe makini pindi anapochota maji sije akamkamata.
Mwantumu alimshukuru Bwana Jumbe na haraka akaendelea na safari yake ya kuelekea mtoni. Aliyakuta maji ni matulivu na vyura walikuwa wakiimba nyimbo za kufurahia maji na hali tulivu ya sehemu ile. Mwantumu kwa tahadhari kubwa akaingza mtungi wake katika maji na ghafla kabla ya kufanikiwa kuchota maji, mamba akamkamata nguo nakuanza kumvutia kwenye maji ya kina kirefu.
Bwana Jumbe hakuwa mbali sana na eneo lile ambalo mamba amemkamata Mwantumu, alikuja huku anakimbia nakupiga kelele, alimkuta mamba amekamata sketi ya mwantumu akiwa ameng'ang'ana kumvutia Mwantumu katika maji marefu. Bwana Jumbe akarukia kwenye maji nakuanza kupambana na mamba yule. Mamba akamwachia Mwantumu na kumdaka Bwana Jumbe mkono.

Je nini kitaendelea? Endelea kufuatilia ujue kama Bwana Jumbe alipona ama la!

Saturday, November 3, 2012

2MTOTO WA MFALME NA LULU

Mfalme alimgeukia mlinzi wake mmoja shupavu na kumwambia kuwa, amepewa jukumu kubwa sana la kuhakikisha kuwa LULU kwaajili ya binti yake inapatikana pia alimwahidi kumpandisha cheo maradufu na kumfanya tu muhimu sana katika familia ya kifalme. Mlinzi Mkwayu alijigamba kuwa atahakikisha anaipata hiyo lulu kwa heshima ya mfalme, basi mfalme alimkabidhi upanga wake wa dhahabu pamoja na chakula chepesi nakumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo.
Mkwayu alipanda farasi wake mweusi mwenye siha njema nakupotea machoni mwamfalme kuelekea katika kisiwa cha Mikwingwina kilichopotakribani kilometa 75 toka pale walipo. Mkwayu kabla yakuondoka alimweleza mfalme angerudi na lulu ndani ya siku 2 zikizidi wajue amepatwa na mabaya. Pia alichoma shale kwenye mti nakuutemea mate yake nakusema ilihali watu wote wakiwa wanasikia maneno yale kwamba, mshale ule ukidondoka wenyewe chini toka katika mti, basi nayeye atakuwa amekumbwa na mabaya huko aendako. 
Usiku wa manane ulivuma upepo mkali sana katika ile sehemu waliyokuwa wamepumzika mfalme na kundi lake mpaka mahema yalikaribia kung'ooka kutokana na upepo uliokuwa unavuma. Mara baada ya dakika takribani arobaini na tano, upepo ulikoma na hali ilibakia katika haliyake ya kawaida. Mlinzi aliyekuwa ameshika zamu usikuhuo alipo kuwa anakagua usalama, alikutana na mshale uliokuwa umewekwa na Mkwayu umedondoka chini, haraka aliwaeleza wenzake na mfalme pia alijulishwa juu ya hali ile na kugundua mojakwamoja kuwa Mkwayu amekutwa na jambo baya huko alikokuwa amekwenda.
Akawaambia walinzi wake kuwa haiwezekani Lulu isispatikane na dhaihiri inaonyesha kuwa huko Mkwayu alipokwenda kunaupinzani mkubwa hivyo waondoke wote waende kuitafuta lulu kwani ingekuwa aibu kubwa sana kwa mfalme kushindwa kupeleka zawadi ya mtoto wake kipenzi Mboni.
Ilipotimia majira ya saa kumi na nusu tayari mfalme pamoja na watu wake walikuwa njiani kuelekea katika visiwa vya mikwingwina ili kumtafutia binti yake mpendwa zawadi aliyo ihiyo ihitaji ya lulu.
Ilipotimu majira ya saa saba hivi mchana mfalme paoja na watu wake walikuwa wamesha wasili ng'ambo yapili ya kivuko kuelekea katika kisiwa cha mikwingwina. Mfalme Mbezi alitoa kifaa maalumu cha kukatisha maji kilichounganishwa na nanga nzito ndogo nakufungwa ng'ambo ya kwanza kisha kufungwa katika kamba ndefu ngumu ya manila nene. Mathayo aliyekuwa mlinzi wa Mbezi alipewa jukumu la kwenda mpaka ng'ambo ya Mikwingwina na kisha kutafuta mtimkubwa afunge kwaajili ya kuvukia juu kwaajili ya mikono na  kamba ya chini kwaajili ya kukanyaga kwa miguu yaani, kwakifupi kitendo cha kufunga kamba ng'ambo ya kwanza na ng'abo ya pili inaitwa NEMA. Baada ya zoezi lile kukamilika Mathayo alirudi ng'ambo ya kwanza ya mikwingwina na kumwambia Mfalme Mbezi kuwa zoezi limekamilika na hali ya kiusalama ipo madhubuti. Mfalme akaamrisha makamanda wawiliwawili wavuke kwenda kisiwani mikwingina kuleta lulu, Sufiani pamoja na Saidi walikabidhiwa vifaa vya kutendea kazi kama kisu cha almasi kwaajili ya kukatia madini ya lulu pamoja na upanga, mkuki pamoja na mishale kwaajili ya kujihami. Saidi na Sufiani walianza safari kwa pamoja mpaka ng'ambo ya pili salama. Walipokuwa njiani kuelekea kaskazini mwa Mikwingwina waliona nyoka aina ya chatu wapatao kama 500 hivi wakawazingira na kuwameza kwa fujo.

Friday, November 2, 2012

MTOTO WA MFALME NA LULU

Hapo zamani za kale, katika kijiji cha Mgombezi, palikuwa na mfalme aliyekuwa anajulikana kwa jina la Mbezi. Watuwake walikuwa hodari sana katika kilimo cha katani pamoja na zao la chakula la mpunga na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Mfalme Mbezi alikuwa pia hodari sana katika kutafuta soko la zao la katani katika nchi za jirani ili kukuza uchumi wa nchi yake. Kutokana na bidii aliyokuwa nayo aliweza kuwa msambazaji mkubwa wa zao la katani katika nchi za Lewa, Manundu, Zavuza nahata Kilole na Kwamatuku. Nchi yake ilikuwa haraka sana kiuchumi na wakaziwake walikuwa wanajiweza vyema kiuchumi. Mfalme Mbezi alisifika ndani na nje ya nchi ya Mgombezi. Alikuwa na jeshi lenyenguvu na watu wake walimpenda sana kwani alikuwa habagui wakumtatulia shida yake au kumsikiliza.
Mfalme Mbezi alikuwa na watoto wawili, wakwanza aliitwa Mjata na wapili aliitwa Mboni. Aliwapenda sana watoto wake, ndio waliokuwa wamebakia pekee na walimfariji sana na hata kusahau kifo cha mke wake aliyekufa miaka miwili iliyopita kutikana na ugonjwa wa kwikwi. 
Sikumoja mfalme aliwaita wanae Mjata na Mboni nakuwaeleza kuwa anataraji kusafiri hivyo wachague zawadi gani waletewe kilammoja pindi baba yao atakapokuwa amerejea toka safari ya nje ya Mgommbezi. Mjata akamshukuru baba yake nakumwambia kuwa angependa aletewe Kanzu nzuri yarangi ya zambarau pamoja na kofia iliyoshonwa kwamwiba wa nungunungu na iwe ya rangi ya zambarau paoja na bakora ya shaba na viatu vya dhahabu. Mfalme Mbezi alivuta pumzi ndefu kisha akamwambia mwanae Mjata kuwa atafanya awezalo ili kuhakikishakuwa anamtimizia hitaji lake. Ikawa zamu ya Mboni kusema zawadi gani aletewe na baba yake pindi atakaporejea toka safari, Mboni akapiga magoti kwaunyenyekevu mbele ya babaye nakumwambia ''Babangu, nitafurahi sana pindi utakaponiletea LULU inayolindwa na jini kisirani katika kisiwa cha mikwingwina, baba nihilo tu hitaji langu'' Mfalme Mbezi alivuta pumzi ndefu kisha akatandikiwa farasi wake nakuondoka na walinzi 12 kuelekea Bungu kisha Lewa kutafuta masoko ya bidhaa ya nchi ya Mgombezi ili kukuza uchumi.
Safari ilichukua siku kumi na kenda na ilikuwa na mafanikio makubwa kwani walipata oda nyingi ya katani na mzigo waliokuwa wamefungasha wa katani pamoja na dhahabu vilikwisha na wakawa napesa nyingi sana. Alianza safari ya kurudi nyumbani lakini mara ghafla alikumbuka ahadi ya zawadi ambazo watoto wake walimtuma. Alinunua kanzu ya rangi ya zambarau ya Mjata pamoja na kofia iliyoshonwa na mwiba wa nungunungu na viatu vya dhahabu. Kazi ikawa kupata LULU aliyo agizwa na binti yake Mboni. Akajiapiza moyoni kuwa hatorudi nyumbani mpaka apate zawadi ya binti yake.

Je! Mfalme atafanikiwa kumpelekea binti yake LULU inayopatikana katika kisiwa cha Mikwingwina na kunajini kisirini anailinda, itawezekana?  Fuatilia kesho.