Monday, July 20, 2015

SITASAHAU MAISHANI.

Nilikuwa darasa latano kipindi hicho, nilikuwa mimi na wadogo zangu wawili. Kawaida yetu ilikuwa kila tukimaliza kula chakula cha usiku tunapumzika kidogo, halafu tunasali, na kama kuna mwenye homework anafanya na anaingia kitandani na kulala. Sikuhiyo baba alikuwa hajarudi kipindi nafanya homework baada ya kuwa tumemaliza kusali na mama pamoja na wadogo zangu walikuwa tayari wamesha lala. Takribani saa sita usiku baba akarudi akiwa chakali amelewa, alibisha hodi mama akaamka na kumfungulia, alikuwa mkali sijawahi kumwona baba yangu akiwa mkali vile, akamnasa mama makofi mbele yangu, mama aligumia kwa maumivu, hali ile iliniuma sana mpaka nikalia. Hakuishia hapo bali alimrushia mateke kana kwamba anapigana na mwanaume mwenzake. Mama aliumia sana, nami sikuweza kuvumilia haliile, kipindi hicho tulikuwa tumeagizwa fimbo za kupeleka shuleni aina ya mikamilwa, nilichukua fimbo mkamilwa mmoja nikamfuata baba aliyekuwa amemwangusha mama chini nakuendelea kumpa makonde yasiyonaidadi. Kwahasira na nguvu nilimtiririshia baba mvua za fimbo mgongoni mpaka nayeye akapiga mayowe. Akamwacha mama na kuanza kunikimbiza, kwakuwa mlango ulikuwa haujafungwa nilitoka mbio nayeye yupo nyuma yangu anakuja mbio anikamate, nikakimbilia sehemu moja iliyokuwa imezibwa njia kwa miiba ya michongoma. Kwakuwa sehemu ile nilikuwa naijua nikairuka miba ile nayeye hakuwa akijua kama kuna miba, aliingia mzimamzima. Alikipata hakika. Nikahamia kwa rafiki yangu wiki nzima na mama akawaomba wazee watusuluhishe mimi na baba. Nilimwomba radhi baba na akanisamehe. Je nisingechukua maamuzi magumu kama hayo mamaangu siangeuwawa mbele yangu namwona?

Sunday, July 19, 2015

MTOTO WA MFALME NA LULU - 3

Mfalme Mbezi alipoona kuwa walinzi wake hawarudi katika siku ileile aliyo wapangia, akaamua aongeze siku moja zaidi kuwasubiria na kama hawatafika aweze kufanya kitu ili kuhakikisha kuwa lulu ya binti yake inapatikana kwahali yoyote ile. Ilipofikia majira ya saakenda mfalme Mbezi alihisi kuwa huenda watuwake waliokuwa wamekwenda kisiwa cha mikwingwina wamep-atwa na mabaya. Akawaambia watuwake waliokuwa pamoja nae kuwa, ''Lulu kwaajili ya binti yangu nilazima ipatikane na sipo tayari kurudi Mgombezi bila lulu'' Akawaambia watu wake kuwa hakuna mtu atakayebakia ng'ambo yakisiwa cha Mikwingwina

WATOTO NI ZAWADI.

Sikumoja Mwantumu alipokuwa amekwenda kuteka maji mtoni, njiani alikutana na Bw. Jumbe ambaye alikuwa anakwenda kuangalia vibuyu vyake vya mnazi kama vimeingia pombe ya mnazi ambayo aliviweka jana alasili. Akamsabahi Mwantumu ambaye alikuwa yupo kwa mwendo wa haraka kidogo kuelekea mtoni. Mwantumu akasimama na kuitikia salamu ya Bwana Jumbe kwa adabu zote. Bwana Jumbe baada ya kusalimiana na Mwantumu, akampa tahadhari kuwa kuna mamba ambaye anashuka kutokea upande wa juu. Hivyo awe makini pindi anapochota maji sije akamkamata.
Mwantumu alimshukuru Bwana Jumbe na haraka akaendelea na safari yake ya kuelekea mtoni. Aliyakuta maji ni matulivu na vyura walikuwa wakiimba nyimbo za kufurahia maji na hali tulivu ya sehemu ile. Mwantumu kwa tahadhari kubwa akaingza mtungi wake katika maji na ghafla kabla ya kufanikiwa kuchota maji, mamba akamkamata nguo nakuanza kumvutia kwenye maji ya kina kirefu.
Bwana Jumbe hakuwa mbali sana na eneo lile ambalo mamba amemkamata Mwantumu, alikuja huku anakimbia nakupiga kelele, alimkuta mamba amekamata sketi ya mwantumu akiwa ameng'ang'ana kumvutia Mwantumu katika maji marefu. Bwana Jumbe akarukia kwenye maji nakuanza kupambana na mamba yule. Mamba akamwachia Mwantumu na kumdaka Bwana Jumbe mkono.

Je nini kitaendelea? Endelea kufuatilia ujue kama Bwana Jumbe alipona ama la!