Friday, November 2, 2012

MTOTO WA MFALME NA LULU

Hapo zamani za kale, katika kijiji cha Mgombezi, palikuwa na mfalme aliyekuwa anajulikana kwa jina la Mbezi. Watuwake walikuwa hodari sana katika kilimo cha katani pamoja na zao la chakula la mpunga na uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Mfalme Mbezi alikuwa pia hodari sana katika kutafuta soko la zao la katani katika nchi za jirani ili kukuza uchumi wa nchi yake. Kutokana na bidii aliyokuwa nayo aliweza kuwa msambazaji mkubwa wa zao la katani katika nchi za Lewa, Manundu, Zavuza nahata Kilole na Kwamatuku. Nchi yake ilikuwa haraka sana kiuchumi na wakaziwake walikuwa wanajiweza vyema kiuchumi. Mfalme Mbezi alisifika ndani na nje ya nchi ya Mgombezi. Alikuwa na jeshi lenyenguvu na watu wake walimpenda sana kwani alikuwa habagui wakumtatulia shida yake au kumsikiliza.
Mfalme Mbezi alikuwa na watoto wawili, wakwanza aliitwa Mjata na wapili aliitwa Mboni. Aliwapenda sana watoto wake, ndio waliokuwa wamebakia pekee na walimfariji sana na hata kusahau kifo cha mke wake aliyekufa miaka miwili iliyopita kutikana na ugonjwa wa kwikwi. 
Sikumoja mfalme aliwaita wanae Mjata na Mboni nakuwaeleza kuwa anataraji kusafiri hivyo wachague zawadi gani waletewe kilammoja pindi baba yao atakapokuwa amerejea toka safari ya nje ya Mgommbezi. Mjata akamshukuru baba yake nakumwambia kuwa angependa aletewe Kanzu nzuri yarangi ya zambarau pamoja na kofia iliyoshonwa kwamwiba wa nungunungu na iwe ya rangi ya zambarau paoja na bakora ya shaba na viatu vya dhahabu. Mfalme Mbezi alivuta pumzi ndefu kisha akamwambia mwanae Mjata kuwa atafanya awezalo ili kuhakikishakuwa anamtimizia hitaji lake. Ikawa zamu ya Mboni kusema zawadi gani aletewe na baba yake pindi atakaporejea toka safari, Mboni akapiga magoti kwaunyenyekevu mbele ya babaye nakumwambia ''Babangu, nitafurahi sana pindi utakaponiletea LULU inayolindwa na jini kisirani katika kisiwa cha mikwingwina, baba nihilo tu hitaji langu'' Mfalme Mbezi alivuta pumzi ndefu kisha akatandikiwa farasi wake nakuondoka na walinzi 12 kuelekea Bungu kisha Lewa kutafuta masoko ya bidhaa ya nchi ya Mgombezi ili kukuza uchumi.
Safari ilichukua siku kumi na kenda na ilikuwa na mafanikio makubwa kwani walipata oda nyingi ya katani na mzigo waliokuwa wamefungasha wa katani pamoja na dhahabu vilikwisha na wakawa napesa nyingi sana. Alianza safari ya kurudi nyumbani lakini mara ghafla alikumbuka ahadi ya zawadi ambazo watoto wake walimtuma. Alinunua kanzu ya rangi ya zambarau ya Mjata pamoja na kofia iliyoshonwa na mwiba wa nungunungu na viatu vya dhahabu. Kazi ikawa kupata LULU aliyo agizwa na binti yake Mboni. Akajiapiza moyoni kuwa hatorudi nyumbani mpaka apate zawadi ya binti yake.

Je! Mfalme atafanikiwa kumpelekea binti yake LULU inayopatikana katika kisiwa cha Mikwingwina na kunajini kisirini anailinda, itawezekana?  Fuatilia kesho.

3 comments: